Saturday, April 28, 2012
Saturday, April 28, 2012
Eti damu ninzito ,
Wanaishi na uongo,
Ukweli utawaua.
Wanaifadhi sura na picha walizo chora kwenye jamii,
Eti wao ni wema, wenye busara,
Eti wao si wakosaji, wanatetea masikini,
Ukweli utawaua,
Ukweli utaua.
Yeye ataki kuku Bali kuwa mwumeye ni mnyama hatari,
Mwanamme anaye iba haki ya uke.
Uongo unakupa amani,
Ukweli utakuua.
Nimesema yaliyonikaba,
nimetema aibu,
Nikakukuta vumbi mwilini,
Uchafu wa mwumeo,
Japo ukakataa
Uka kumbatia simba aliye mega wakwako,
Nimejifunza kukaza mwendo,
Nawaonea huruma,
Najua ukweli utawaua,
Ndomana mkanikataa,
Mkatetea simba aliye mla wankwenu.