Nimetoe Posa

Saturday, April 28, 2012

 

Nimetoa posa,

Nimekutolea posa,

Mwanangu umekuwa,

Mwanangu umechukuliwa,

Mwanangu umenunuliwa


Nimetoa posa,

Nimekutolea posa,

Mama shule sijamaliza,

Posa nisitolewe,

Mimi nisiolewe


Nimetoa posa,

Nimekutolea posa,

Mtoto wewe utaolewa,

Acha matope,

Nenda kaoge upendeze,

Juma kakupenda,

Mchumba umepata,

Mwanangu umenunuliwa,

Mwanangu Juma anakuchukuwa.


Nimetoa posa,

Nimekutolea posa,

Mama vipi kuhusu elimu,

Mwalimu kasema naweza kufika mbali,

Hesabu nazijua,

Ninacho hitaji ni mda, sikumoja naweza kuwa mtu mkubwa,

Mama nitakujengea nyumba,

Kijiji utakiacha,

Utatoroka shamba,

Tuta mtoroka baba,

Utatoroka mateke na vipigo vya fimbo za migamba,

Mama kataa posa,

Mama mimi mdogo kununuliwa,

Mama mimi mdogo kuolewa.


Nimetoa posa,

Nimekutolea posa,

Mtoto ziache ndoto,

Mwanamke azaliwe,

Alewe,

Akito matiti na ungo kuvunja,

Ndani awekwe,

Afwenzwe kulea mwemu,

Hebu acha hayo makaratasi,

Hifadhi hiyo kalam,

Hiyo siyo ya kwako tena, hiyo ni ya kaka yako.



Nimetoa posa,

Nimekutolea posa,

Mama Juma simtaki,

Tafadhali niombee ruksa kwa baba,

Niende kuishi na shangazi,

Nitamwonyesha baba,

Kuwa mtoto wakike sio hasara,

Nitahifadhi pesa, nitawatunza,

Nakuhahidi amto teseka,

Mama rudisha posa,

Mama usinioze,

Mama usiniuze.



Nimetopa posa,

Nimekutolea posa

Mwanamke kazi yake nyumbani,

Elimu yake jikoni,

Ujuwe kuwa ugali an ndimu hacienda,

Napo  jua likienda kulala,

Mwenzi ukiangaza,

Hakikisha kiuno wakiregeza,

Kinyonge,

Kitake,

Kinyonge,

Mweke mwume chumbani,

Asiende kulala na wanje,

Akilia mwume, mbembeleze na mzalie madume.

Mwanangu umetolewa posa,

Mwanangu juma Kaukauna,

Mwanangu juma atakuchukua.

 
 

next >

< previous

To reach Queen:
Queen can be reached to schedule speaking engagements by emailing Queen at:
Queen@antosca.commailto:Queen@antosca.comshapeimage_4_link_0